Zoezi la kupokea watumishi wapya limeanza leo tarehe 1/7/2021 Ikiwa ni siku ya kwanza ya mwaka mpya wa fedha 2021/2022.
Jumla ya watumishi kumi na saba (17) wameripoti sawa na 16.8%. ya watumishi walipangiwa Kongwa ambapo 13 kati yao ni walimu, na wanne ni watumishi wa Afya.
Wakizungumza na Ofisi ya Habari, watumishi hao wameeleza kufurahishwa na utaratibu wa mapokezi unaozingatia utu na matumizi ya muda.
Mwalimu Godson Geofrey Molla amethibitisha kuridhishwa na mchakato mzima wa mapokezi na ameshauri watumishi wapya kuripoti mapema ili kurahisisha zoezi kwa maafisa wanao shughulika na zoezi hilo.
Upande wake Daktari Samwel Masanja, ameshauri watumishi kuripoti na kwenda kwenye vituo vya kazi badala ya kuripoti na kuondoka.
Naye Katibu Msaidizi wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Wilaya ya Kongwa Ndugu Edward Chamwela amewakumbusha Walimu wapya na watumishi wengine Kuja na vyeti halisi na vivuli vyake, kitambulisho cha Taifa na picha 5 za ‘’Passport size’’ili kuepuka usumbufu.
Ameongeza kuwa walimu wapya ni lazima wazingatie Haiba ya ualimu kuhusu Mitindo ya mavazi, Nywele, na Matumizi ya lugha.
Tukio la mapokezi limeshirikisha wadau mbalimbali wanaofanya kazi kwa ukaribu na Halmashauri ya Kongwa vikiwemo vyama vya wafanyakazi, TSC, PSSSF na NMB tawi la Kongwa, ambao wanasajili wateja wapya wasio na Akaunti za Benki. Zoezi hilo linalosimamiwa na Idara ya Utumishi na Utawala linatarajia kudumu kwa muda wa wiki mbili.
Stephen Jackson - Kongwa
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.