Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Suleiman Jafo amefanya ziara ya ghafla Wilayani Kongwa ambapo ametembelea Kituo cha Afya Mlali kukagua ujenzi unaoendelea wa Kituo hicho. Kituo hicho kimepokea shilingi milioni mianne (TSh. 400,000,000/-)ambazo zimetolewa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Uongozi wa Dkt. John Pombe Magufuli.
Katika ukaguzi huu Waziri Jafo amepongeza kazi nzuri na kuwataka Viongozi wa Halmashauri, Mkurugenzi Mtendaji na Menejimenti yake kusimamia vema kazi ili ikamilike vizuri.
Ujenzi wa Kituo hicho uko mbioni kukamilika ambapo unajumuisha ujenzi wa majengo matano; Nyumba ya Mtumishi, Wodi ya Mama na Mtoto, Maabara (Laboratory), Upasuaji (Theater), na Ulazaji Maiti (Mortuary).
Katika ziara hiyo alikuwepo pia Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Deogratius Ndejembi.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.