Katika Mkutano wa Baraza la Madiwani Wilaya ya Kongwa, Changamoto ya Huduma za Jamii zikiwemo huduma za Afya na Elimu zimechukua nafasi kubwa ya mjadala katika Mkutano wa Robo ya tatu Mwaka wa Fedha 2017/18 kilichofanyika Katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa tarehe 24-05-2018.
Madiwani wa Kata ya Iduo, Songambele, Chitego na Pandambili walielezea changamoto za Huduma ya Afya zinazofanana ikiwemo kukosekana kwa dawa muhimu zikiwemo Paracetamol, mipira ya kuvaa mikononi (Gloves) kwa ajili ya kuhudumia akina mama wakati wa Uzazi Katika vituo vya Afya na Zahanati.
Changamoto nyingine kubwa iliyojadiliwa ni upungufu wa Walimu na Wahudumu wa Afya kwani kuwepo kwa mhudumu mmoja-mmoja katika vituo vingi vya Afya ni hali inayodhoofisha huduma za Afya na hupelekea wakati mwingine huduma kukosekana, mtumishi huyo anapopata likizo, dharula za kikazi au kuugua.
Aidha, Diwani wa Kata ya Mlali Mhe Richard Mngurumi alisema Zahanati ya Kijiji cha Ihanda imefungwa kutokana na watumishi walio kuwepo; mmoja aliondolewa kwa vyeti vya kugushi na mwingine aliomba uhamisho kama haki yake. Hivyo, anaiomba Serikali kuisaidia Kata hiyo kwa kupeleka mhudumu katika kituo hicho cha ili kuwasaidia wananchi wa kijiji hicho kutatua matatizo yao ya kiafya.
Mwenyekiti wa kamati ya Huduma za Jamii Diwani wa Kata ya Msunjulile Mhe. Chilingo Chimeledya amekiri kuwepo kwa Zahanati ambazo hazijafunguliwa na ameliambia Baraza Zahanati hizohazijafunguliwa kutokana na sababu ambalo zipo nje ya uwezo kutokana na Kutokuwa na wahudumu wa kuhudumia katika Zahanati hizo.
Hivyo, katika Zahanati ya Ihanda Halmashauri kupitia Idara ya Afya itafanya utaratibu mhudumu apatikane ili ifunguliwe; Pia, Serikali itakapoajiri kutakuwa na kipaumbele kwa Zahanati, vituo vya Afya na Shule zenye upungufu wa walimu.
Aidha, kufuatia changamoto za elimu wilayani Kongwa ikiwemo upungufu wa Madarasa na Vyoo, Baraza limeridhia hoja ya uanzishwaji wa Mfuko wa Elimu wa Wilaya ambao utakusanya fedha na kuwekwa katika akaunti za Kata.
Akiwasilisha Taarifa ya Kamati katika Mkutano wa Baraza la Madiwani Mhe. Chimeledya alisema, Mwenyekiti wa Kamati za Huduma za Jamii ameeleza kwamba Kamati ilishauri kila mwananchi mwenye umri wa miaka 18 atapaswa kuchangia TShs.10,000/= kwa mwaka ambapo fedha hizo zitatumika kutatua Changamoto za kielimu Katika kila Kata.
Kadhalika, Kamati ya Huduma za Jamii ilishauri viongozi wa Kata watumike kuhamasisha na kuhimiza wananchi kutoa michango hiyo, pia viandaliwe vitabu vya stakadhi za malipo, wakabidhiwe watendaji Vijiji na Kata vikiambatana na onyo kali juu ya ubadhilifu wowote utakajitokeza.
Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo Kibaigwa Mhe. Samweli Mganga ameiomba Serikali kuhakikisha inafanya usajili kwa shule za mkondo zilizotimiza vigezo ili kuondoa adha ya umbali wa shule kwa wanafunzi na kuwangezea ari ya Kusoma.
Pia, Diwani wa Kata ya Hogoro Mhe. Drank Mgata ameitaka Halmashauri hiyo kupeleka mwalimu wa Kike Katika Shule ya msingi Mkutani kwani kuna walimu wa kiume tupu ili kuwasaidia wanafunzi wa kike wanaopevuka ambapo kuelekezwa na walimu wa kiume ni kinyume na mila na desturi za kiafrika.
Sambamba na Changamoto hizo kuchukua nafasi kubwa Katika mjadala Kikao hicho kilijadili mambo Mbalimbali yakiwemo ya kiuchumi, Mazingira, na udhibiti wa maambukizi ya Ukimwi ambapo Mwenyekiti wa Kamati ya Kudhibiti maambukizi ya UKIMWI Diwani wa Kata Ya Mkoka Richard Mwite amewataka Madiwani kuhamasisha wananchi upimaji wa VVU Hiari.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.