Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina awasha moto kwa unongzi unaosimamia ranchi ya taifa (NARCO) iliyopo Wilayani Kongwa. Katika ziara yake Desemba 1, 2017 ameutaka uongozi huwa kufanya ufyugaji wa kisasa zaidi wenye tija ambao utaleta manufaa kwa taifa na wanachi kwa ujumla.
Aidha, alishangazwa na utumiakaji wa eneo dogo la malisho la ekali 3,000 wakati ranchi hiyo ina ukubwa wa ekali 38,000. Hivyo, amemuagiza Mkurugenzi wa ranchi hiyo ya Taifa iliyokubwa hapa nchini kuboresha mazingira ya ufugajim kwa kuongeza eneo la malisho kutoka ekali 3,000 za sasa hadi kufikia ekali 38,000. Sanjari na hilo, ameagza uongozi huo wa ranchi kuongeza idadi ya mifugo kulingana na eneo lilivyo, hivyo amemtaka mkurugenzi wa ranchi kufanya jitiada za kufikisha idadi ya ng'ombe 20,0000 ifikapo desemba mwaka 2018.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.