Utangulizi:
Jengo la Kituo cha Biashara ni miongoni wa miradi ya kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji unaotekelezwa katika Halmashauri ya Kongwa. Ujenzi huu ulifadhiliwa na Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji - Local Investment Climate project (LIC). Ujenzi wa mradi wa kituo cha kibiashara ulianza tarehe 1/02/2016 na kukamilika tarehe 30/6/2016 eneo la Uzunguni Kiwanja Namba 11 block A lenye ukubwa wa 1710M2
Mradi huu umegharimu jumla ya Tshs. 101,539,912/= ambapo LIC wamegharamia ujenzi wa jengo Tshs. 67,111,000, usimamizi na ukaguzi wa ujenzi Tshs 2,384,500 na thamani za ofisini Tshs. 15,465,000, Mfumo wa utoaji huduma katika Kituo ni Tshs.12,123,912 na mchango wa Halmashauri ni kiwanja chenye thamani ya Tshs.6,840,000.
Watumishi Watakaotoa Huduma katika Kituo hiki (OSBC):
Lengo la Kituo:
Lengo la ujenzi wa jengo hili ni kutengeneza mazingira bora ya upatikanaji wa huduma ya leseni ya biashara kwa kuondoa mlolongo wa upatikanaji wake, pia utoaji wa taarifa mbalimbali za masoko ndani ya Wilaya na utoaji huduma ya risiti kwa njia ya kielektroniki.
Wanufaika wa mradi huu ni wafanyabiashara, wawekezaji na Halmashauri ya Wilaya.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.