Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira Mhe Antony Mavunde amezindua rasmi kampeni ya upandaji miti Wilayani Kongwa jana, Januari 25, 2018 katika maeneo ya chini ya safu ya milima Kiboriani eneo la Kijiji cha Ibwaga.
Katika uzinduzi huo, Mhe Mavunde amewataka wananchi wa Kijiji cha Ibwaga kuleta mabadiliko ya kifikira katika kuufanya Mkoa wa Dodoma kuwa wa kijani kwa kupanda miti na kutunza mazingira ili kuongeza fursa za kiuchumi ikiwemo za kilimo na ufugaji wa nyuki.
Mhe Mavunde amewataka wananchi hao wajitolee kuunda vikundi vya utunzaji wa mazingira ili viweze kufaidika na Mfuko wa Misitu Tanzania Forest Fund (TFF) unatoa ruzuku ya utunzaji wa misitu ili kuweza kujiinua katika fursa za kiuchumi ikiwemo ufugaji wa nyuki na katika mazingira hayo wanayoyatunza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara, Dkt John Magufuli, Machi 19, 2018, ameongoza Mkutano wa 11 wa baraza hilo, Ikulu jijini Dar es Salaam.Dhumuni la Mkutano huo ni kujadili mambo mbalimbali yanayohusu sekta ya biashara nchini, na namna ya kutatua changamoto zinazoikwamisha sekta hiyo kuendelea kuku na kupanuka kimataifa zaidi.Kauli mbiu ya baraza hilo ni “Tanzania ya viwanda - ushiriki wa sekta binafsi”.
Aidha mkutano huo umehudhuriwa na Wafanyabiashara Mashuhuri nchini akiwemo, Mohamed Dewji 'MO', Mkurugenzi wa IPP Reginald Mengi, Said Salim Bakhresa na wengine wengi. (Chanzo: Global TV Online)
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.